Highlight » Baadhi ya Comments za Majaji…
Baadhi ya Comments za Majaji…

Washiriki wa BSS top 7 wiki ya jana walikuwa kwenye kazi ngumu pale ulipotakiwa kuimba wimbo toka kwa chaguo la mshiriki mwenzako.
Show ilianza pale alipofungua pazia mshiriki toka Dar Kelvin Mbati kupanda jukwaani na wimbo wa Kwa ajili yako toka kwa Hussein Machozi ambapo toka kwa majaji hakupata Comments nzuri kwani wote kwa pamoja walisema aliuimba wimbo kama ulivyo lakini hakuweza kumfikia Hussein Machozi mwenyewe.
Ndipo akaingia Catherine Ntepa na wimbo wa Jamila toka kwa gwiji la muziki nchini Uganda, kusema kweli Catherine alionyesha kubabaika na wimbo huo sijui kutokana na tumeshamzoea akiimba kiingereza zaidi siku za nyuma, majaji nao hawakuwa nyuma, P Funk alisema leo umeboronga kuanzia matamshi ya maneno, ilikuwa tofauti kwa Salama ambaye alimrekebisha P Funk kwa kumwambia kuwa kama haelewi ni kuwa Catherine amezaliwa Zambia kusoma na kukulia Zambia, Master Jay yeye alisema kuwa ni Mkali, Madame akasema anamkubali.
Alifuatia Jackson na wimbo wa Hemed "Wakati mwengine" ambapo kama ni kushangiliwa alishangiliwa sana na watazamaji waliofika kwenye studio zetu pale mikocheni, ndipo ikafika zamu ya majaji ambapo P Funk alisema ya kuwa wimbo ni wa kawaida kabisa.
Walifuatia Mary Lucos, Paschal Cassian aliyepanda na wimbo wa Mchizi Mox "Mambo vipi" na Peter Msechu ambaye alipanda na wimbo wa Mtoto Iddi toka kwa Juma Nature ambaye alisifiwa na majaji ya kuwa anaweza kufanya show.

