Highlight » BSS Second Chance is ON – The First Episode
BSS Second Chance is ON – The First Episode
BSS Second Chance imeanza rasmi kwa washiriki 14 kuingia ndani ya Academy ambayo itakuwa chini ya Mwalimu maalum kwa kipindi chote ili kuweza kuwafanya washiriki kuingia kwenye soko la Kimataifa.
Chini ya Majaji watatu maarufu wakiongozwa na Chief Jaji Madame Rita, Salama Jabir, Master J, wataweza kuwasikiliza washiriki wote baada ya hapo kutoa comments zao na kutaja ni nani atabaki na nani atoke “ASEPE”
Chini ya Mwalimu Noah Omolo washiriki 14 watakaoingia ndani ya Academy watakuwa chini ya uangalizi wake.
Noah Omolo ambaye ni mwalimu Mkuu wa Academy alisema zaidi ya kuwafundisha muziki washiriki pia atawafundisha nidhamu ya muziki, aliweza kuwahakikishia Watanzania ya kuwa ana uhakika washiriki hao watakapotoka watakuwa ni wanamuziki wakamilifu kabisa na kuwa tayari kuingia kwenye soko la muziki wa kimataifa.
Kwa upande wa Majaji wao wanaelezea nini kuhusu second chance juu ya washiriki wote.
“The Second Chance tunataka kumpa mshiriki nafasi nyingine tena kwa mara ya pili katika maisha yake” alisema Chief Judge Madame Rita
Naye Master Jay yeye hakuwa na mengi ya kusema juu ya washiriki mwaka huu kwa kuwaambia “Tuko KIKAZI zaidi”
Salama Jabir Jaji anayejulikana kwa kwa kuwapasha ukweli washiriki yeye alisema “Michuano ya Mwaka huu itakuwa ya kukata na shoka”
