Highlight » BSS Second Chance wapagawisha Mwanza
BSS Second Chance wapagawisha Mwanza
Friday September 30, 2011 7:14 AM BT

BSS Second Chance wapagawisha Mwanza
Ilikuwa ni siku ya furaha kwa wakazi wa Mwanza pale walipopata wasaa wa kuwaona Jukwaani washiriki wa BSS Second Chance 2011.
Ilikuwa ni moja ya tamasha la kufunga mwaka ndani ya Jiji la Mwanza ambapo washiriki wote kwa pamoja walipanda jukwaani kutumbuiza.
Hajji Ramadhan ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wa wa wasanii wenzake alipanda jukwaani na kuanza kuwakaribisha washiriki wengine.
Furaha ya wakazi wa Mwanza ni pale alipopanda Beatrice William na Hajji Ramadhan ambapo walipagawisha kupita kiasi na kupokewa na wananchi wa Mwanza.
Wengine waliotia fora ni Chiby Dayo na Bella Kombo.
