Highlight » BSS Second Chance watembelea Kituo cha Watoto Yatima

BSS Second Chance watembelea Kituo cha Watoto Yatima

Monday September 05, 2011 10:32 AM BT

image

BSS Second Chance watembelea Kituo cha Watoto Yatima

Washiriki pamoja na Majaji wa BSS Second Chance walitembelea kituo cha Watoto yatima cha Maunga kilichopo Kinondoni Hananasif.

Wakiwa kituoni hapo washiriki kwa pamoja walipata wasaa wa kuzungumza na walezi pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo hicho.

Jaji Mkuu ambaye pia ni mkurugenzi wa benchmark Production Madame Rita alisema moja ya kazi kubwa ya kampuni yake ni kuwa karibu na Jamii na kushiriki kwenye kazi za Jamii na kwakuwa shindano la Bongo Star Search ni la Watanzania wa Umri wote basi wanayo furaha kufika kwenye kituo hicho.

Zaidi ya hayo Madame Rita alitoa kiasi cha hela za Kitanzania Shilingi Milioni Moja (1,000,000/-) kama msaada kwa kituo hicho na kuahidi kuwa mlezi wa Kituo hicho.

Furaha ya Watoto hao iliongezeka pale washiriki wote walipokula chakula na kuimba kwa pamoja, na furaha yao ilikamilika alipoimba Madame mwenyewe.

Bongo Star Search Second Chance haikuwepo wiki iliyopita kutokana na kuwapa nafasi washiriki kwenda kusheherekea na familia zao.

Endelea kumpigia kura mshiriki wako kwa kuandika namba ya ushiriki na kisha kutuma kwenda 15747



Comment on this Highlight