Highlight » BSS Second Chance yashika Moto

BSS Second Chance yashika Moto

Tuesday August 30, 2011 4:21 PM BT
image

image

Ikiwa iko katika hatua ya nane bora washiriki wa Bongo star Search Second Chance wamesimama na kutoa maoni yao kuhusu mashindano yanavyoendelea.

Wakiongea kwa nyakati tofauti katika usiku wa Flava Nite pale Mzalendo Pub washiriki walikubali ya kuwa mashindano ni magumu lakini wote kwa pamoja wakasema wako fresh kukabiliana na ugumu huo.

“Sikatai mwaka huu ni mgumu kuliko hata mwaka niliyokuwepo, watu wanakaza ile mbaya, lakini naamini siku moja kitaeleweka tu” alisema Bella Kombo mmoja wa washiriki wakali na mwenye vituko.

Naye Kiongozi wa nyumba wa wiki hii Waziri Salum alisema “ Mashindano ni magumu asikuambie mtu, lakini naamini katika wapiga kura wangu kuwa hawataniangusha kabisa na mimi sitawaangusha napenda kuwaambia” alisema Waziri



Comment on this Highlight