Highlight » BSS Waendelea kutesa Arusha

BSS Waendelea kutesa Arusha

Thursday October 06, 2011 4:39 AM BT


BSS Waendelea kutesa Arusha

Washiriki wa Nne wa BSS Second Chance 2011 waliendelea na ziara yao ya mikoani kwa kufanya Show Mjini Arusha Mwisho wa Wiki Hii.

Ilikuwa ni show ya aina yake pale washiriki hao walipopanda jukwaani na kufanya kile kilichotarajiwa na wengi.

Onyesho hilo lilifanyika katika ukumbi wa Tripple A ambapo ulisheheni umati wa watu kufikia wengine kushindwa kuingia.

Wakiongea na Bongostars.com washabiki wa Arusha ambao walifika kwenye onyesho hilo walisema walikuja kuwaona na kuburudika na wasanii hao kabla ya kuwapigia kura siku ya mwisho wa Fainali.

“Nimewaona na nimeshajuwa nani nitampigia kura, na pi anime-enjoy sana kuwaona Live siku zote nawaona kwenye TV tu” alisema Angela wa USA River

Hilo ndilo lilikuwa onyesho la mwisho kwa nje ya Mkoa kwa BSS Second Chance kabla ya Fainali.



Comment on this Highlight