Highlight » Chini Ya Kapeti

Chini Ya Kapeti

Tuesday September 13, 2011 6:37 PM BT

image

Chini Ya Kapeti

Habari za Mpya kabisa za Chini ya Kapeti eti ni kuwa Mary Lucos na Shafii ni Wapenzi kweli kweli kabisaaaa.

Wawili hao waliweka wazi wiki hii pale kwenye fukwe za Mbalamwezi mara baada ya kukutwa ZERO DUSTANCE, Ili kutaka kujuwa nini kinaendelea bongostars.com kama ilivyo ada ya umbea wake ilisogea karibu na wapenzi hao na kuuliza kulikoni?

“Alianza Shafii ambaye alikuwa ni mmoja wa washiriki kujibu “Nimekuja kumpa Mama Sapoti si unajuwa tena mambo si siri tena kila kitu hadharani sasa” alisema Shafii

Bila kusita ilibidi tumtafute Mary ambaye naye alikiri ya kuwa ni kweli hakuna la kuficha Shafii ni Mchumba wake na kila kitu kinakwenda sawa kabisa.

“Nampenda sana Shafii, na huyu ndiye Mr Wangu kama ulikuwa hujui” alisema kwa kujigamba kabisa Mary.

Kweli BSS ni Nomaaaaa, zaidi ya Zawadi Kibao hata Wachumba pia humo humo.

Shafii na Mary wote wameshatolewa kwenye mashindano ya Mwaka huu.



Comment on this Highlight