Highlight » Endelea Kumpigia Kura mshiriki wako
Endelea Kumpigia Kura mshiriki wako

Macho na Masikio ya Watanzania wote wapenzi na washabiki wa BSS yataelekezwa wiki hii ili kupata kujuwa ni nani na nani wameingia Fainali pale kitendawili kitakapoteguliwa ndani ya show ya wiki hii.
Ikiwa ndio tunaelekea Fainali basi muokoe mshiriki wako kwa kumpigia kura nyingi uwezavyo ili awe mmoja watakaoingia ndani ya fainali baadae.
Wiki hii tulishuhudia washiriki Beatrice William, Catherine Ntepa, Mary Lucos wakiingia ndani ya Danger zone ambao kati yao hao wawili ndio watakaoga mashindano ya mwaka huu na mmoja kuungana na wanaume waliobaki ambao wana uhakika wa kuingia Fainali za mwaka ambao ni Jackson George, Paschal Cassian na Kelvin Mbati.
Basi ni kazi yako mwananchi kuhakikisha unapiga kura nyingi uwezavyo kumuoakoa mshiriki unayempenda kwa kuandika neno BSS namba ya Mshiriki halafu unatuma kwenda namba 15550.

