Highlight » Hodi Hodi Tanga Eid El Fitr..

Hodi Hodi Tanga Eid El Fitr..

Thursday July 29, 2010 1:55 PM BT
Wakazi wa Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake mwishoni mwa wiki hii yani siku ya Eid Mosi watashuhudia ile top seven ya Bongo Star Search wakivamia jijini humo tayari kwa mashambulizi makali....

image

Wakazi wa Mkoa wa Tanga na vitongoji vyake mwishoni mwa wiki hii yani siku ya Eid Mosi watashuhudia ile top seven ya Bongo Star Search wakivamia jijini humo tayari kwa mashambulizi makali.

Bongo Star Search inawaomba wakazi wa Tanga na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi zaidi tayari kushuhudia show kali kabisa ya mwaka.

Washiriki watakaoondoka kuelekea Tanga kuangusha show hiyo ni Beatrice William, Kelvin Mbati, Mary Lucos, Jackson George, Catherine Ntepa, Peter Msechu na Pascal Cassian.

Zaidi ya hapo kutakuwa na yule mkali wa show za Michael Jackson (Sabaha Jackson) ambaye ameahidi bonge la suprise toka kwa wapenzi wote watakaojitokeza siku hiyo.

Show itafanyikia uwanja wa Mkwakwani na Kiingilio ni wakubwa sh elfu Mbili (Tsh 2000/-) na watoto itakuwa ni sh elfu moja (Tsh 1000/-)



Comment on this Highlight