Highlight » Majaji Wazungumza kuhusu Mashindano
Majaji Wazungumza kuhusu Mashindano

Majaji Wazungumza kuhusu Mashindano
Majaji wakuu watatu ambao ndiyo wanatoa maoni pamoja na kuwarekebisha washiriki wa BSS Second Chance, Chief Judge (Madame Rita), Salama J na Master Jay wameongea na mtandao Mama wa BSS Second Chance 2011, bongostars.com na kutoa maoni yao juu ya mashindano ya mwaka huu.
Akiongea nasi Chief Judge alisema mashindano ni magumu kutokana na ushindani uliopo baina ya washiriki.
“Angalia washiriki wa mwaka huu walivyowakali, kusema kweli inapelekea hata sisi kuwa na wakati mgumu katika kuchagua na ndiyo maana tukawaachia Watanzania waamue wenyewe kwa kupiga kura, mi nadhani ni moja ya Mashindano Bora kabisa kuwahi kutokea” alisema Madame Rita.
Naye Salama J ambaye anaeleweka na Wananchi kutokana na kupasua ukweli moja kwa moja pale inapobidi hata kwa upande wake alikubali ya kuwa mashindano ni magumu.
“Mashindano ni magumu hata wewe mwenyewe si unaona, Vijana wako fit naona wamesikia Mkwanja uliopo mbele yao kwahiyo hawataki kufanya makosa kwasababu hii ni Second Chance” alisema Salama J
Naye Master J alisema “Vijana ni WAKALI ile mbaya ni makosa madogo tu ya kiufundi ambayo yanarekebishika kabisa bila tatizo wakiingia studio, tutawafundisha, mimi naongelea Technical kuwa ni vitu vidogo” alisema J
Kuendelea kumpigia kura mshiriki wako tuma Namba ya mshiriki kwenda 15747
