Highlight » Mary aaga Mashindano
Mary aaga Mashindano

Mshiriki Mary Banyukwa mmoja wawashiriki wakali kabisa katika shindano la Mwaka huu ameyaaga Mashindano ya Bss Second Chance baada ya kupata kura Chache.
Mary ambaye alikuwa kwenye Danger Zone wiki mbili mfululizo alipata kura chache kuzidi za mwenzake waliyekuwa nae Danger Zone Imani Lissu.
Akiongea mara baada ya kutajwa kwa Jina lake Mary alisema kwenye ushindani wowote lazima kuna kushinda na kushindwa hivyo basi anayakubali matokeo yote kwa moyo mmoja.
‘Nawapenda kuwashukuru Watanzania kwa Kunipigia Kura na kunifikisha mpaka hapa, napenda kuwashukuru Benchmark kwa kutambua umuhimu wangu, napenda kuwausia wenzangu wakaze Buti mashindano ni magumu lakini naamini wote wanaweza’ alisema Mary
Shindano la BSS mwaka huu mpaka sasa washiriki wamebaki nane (9).
Wiki hii walioingia Danger Zone ni Imani Lissu na Sarafina Mshindo.
Endelea kumpigia kura mshiriki unayeona anafaa kuwa BSS Second Chance Winner 2011 kwa kupiga kura yako kuituma kwenda 15747
