Highlight » Milioni 55 Kutolewa kwa BSS Second Chance WINNER
Milioni 55 Kutolewa kwa BSS Second Chance WINNER

Mkurugenzi wa Benchmark ambaye pia ni Jaji Mkuu Madame Rita alitangaza zawadi za washindi wa BSS Second Chance kwa Mwaka 2011.
Mbele ya Waandishi wa Habari Chief Judge alisema kuwa zawadi za washindi kwa mwaka huu ni Tsh Millioni 55 ambapo zitagawiwa kwa washindi watano bora wa Kwanza.
"Nia yetu ni kuwasaidia hawa vijana kujikwamua kimaisha kwa maana hiyo kutokana ukubwa wa zawadi kwa mwaka huu tumeonelea kuwa tusiwaache na wengine hivyo basi katika Milioni 55 zitakazotolewa tumejaribu kuzigawa ili na wengine pia waweze kujiona ni moja ya washiriki wakali" alisema Chief Judge.
Chief Judge aliwashukuru wadhamini wote kwa kufanikisha BSS Second Chance 2011 kwa hali moja ama nyingine.
Washiriki waliobaki mpaka sasa ni Sarafina Mshindo, Hajji Ramadhan, Chiby Dayo, Bella Kombo, Imani Lissu, Mary Lucos, Beatrice William, Waziri Salum na Rogers Lucas.
Kuendelea Kumpigia Kura mshiriki wako tuma namba ya mshiriki kwenda 15747