Highlight » Mwanza Mwanza - Ni Hajji Ramadhan
Mwanza Mwanza - Ni Hajji Ramadhan

Hatimaye kile kitendawili cha Nani Mkali katika BSS Second Chance 2011 kwa taji kwenda kwa mara nyingine tena kanda ya Ziwa pale mkali wa mauno viuno Hajji Ramadhan kutangazwa mshindi.
Fainali ya mwaka huu ambayo kila mmoja ukumbini aliondoka akiwa roho nyeupe kabisa kutokana na kuridhishwa na ushindi huo.
Show ilianza kama kawaida kwa washiriki wote kujinadi mbele ya watazamaji kwa kuimba nyimbo walizozichagua wenyewe.
Alianza Salum Waziri ambaye alipanda jukwaani na kuomba kura kwa kuimba nyimbo ya zamani kama ilivyo ada ya shindano lenyewe, akafwatia Rogers Lucas, Hajji Ramadhan kisha akamaliza mwanadada pekee aliyebaki kwenye mashindano hayo alimaliza.
Show ilisindikizwa na wakali wengi akiwepo Flavor toka Nigeria, Navio toka Uganda na wakali wengine wa hapa hapa nchini kama Mr Flava a.k.a Sharobaro.
Ila kivutio kikubwa alikuwa ni pale alipopanda mmoja wa washiriki wa mwaka Jana Kijana Joseph Payne alifunika na wimbo wake wa Ruka toka kwa kundi la Tip Top Connection ambapo alishangiliwa na ukumbi mzima.
Hajji Ramadhan anakuwa mshindi wa pili toka Mkoa wa Mwanza baada ya mwaka Juzi mkoa huo kumtoa Pascal Cassian.
Kwa maana hiyo Hajji Ramdhan anajinyakulia kitita cha TSH Milioni 45 kwa kushinda shindano hilo.
Endelea kutembelea website yetu uweze kupata show nzima ilivyokuwa kupitia Video
