Highlight » Mwapwani Yahaya aaga Mashindano

Mwapwani Yahaya aaga Mashindano

Monday August 15, 2011 10:11 AM BT
image

image

Ilikuwa ni wiki ya nyimbo za Disco kwa washiriki kila mmoja kuchagua wimbo ambao ataona unamfaa chini ya mwalimu na mlezi wa Academy Mwalimu Noah.

Washiriki wote walijitahidi kuchagua nyimbo zilizoendana na wao wenyewe, Waziri Salum yeye akiimba ‘Find Your Love’ wa Drake, wakati Chiby Dayo alipanda na ‘Kuch Kuch Hotae’, Imani Lissu akipanda na wimbo wa Michael Bolton ‘How am I supposed to Live’ basi kila mmoja akitimiza wajibu wake.

Washiriki walipendeza kama kawaida, Huku wakiwa na nyuso za wasiwasi kwani mmoja wao ilikuwa ni lazima achape Lapa siku hiyo, washiriki walijitahidi kuimba kwa uwezo wote huku majaji wakiwapa comments tofauti tofauti.

Washiriki walioingia kwenye Danger Zone kwa wiki hii ni Imani Lissu na Mary Banyukwa Wakati aliyeaga mashindano alikuwa ni kutoka Dodoma Mwapwani Yahaya.

Endelea kumuokoa Imani Lissu na Mary Banyukwa kwa kuwapigia kura kutuma number ya ushiri wao kwenda 15747



Comment on this Highlight