Highlight » Na Wale TOP 14 Wetu ni…

Na Wale TOP 14 Wetu ni…

Thursday July 21, 2011 1:01 AM BT

image

Ndipo ulipoanza mchujo wa washiriki wote kuingia ukumbini pale katika Hotel maarufu ya Paradise Express kwa kila mmoja akienda kujinadi mbele ya Majaji kwa washiriki wote ishirini waliofika ishirini Bora (Top 20).

Alianza Faisal Ismail kujinadi mbele ya Majaji ambapo alipoulizwa imekuwaje kwenye chumba ambacho kilijulikana kama chumba cha sindano aliweza kusema “Mzee nasikia tumbo Joto”.

Beatrice William toka pande za Mwanza kama unamkumbuka alitokea kuibamba sana BSS ya mwaka 2009 naye aliingia kwenye chumba cha sindano, yeye alisema “ni kawaida tu”.

Bella Kombo mshiriki ambaye mwaka jana aliweza kuibamba kinoma BSS 2010 alikiri ndani kule ilikuwa tumbo joto lakini anajiamini kwamba anatisha.

Walifuatia wengine wote 20 waliokuwamo kama vile Lucas Rogers, Immani Lissu, Waziri Salum, Lulu Abdul na wengine wote.

Sasa ndiyo ukafika ule muda wa Majaji kufikia uamuzi wao wa nani asepe na nani abaki kuingia kwenye Academy.

Washiriki wote walikuwa kwenye hali ya wasiwasi kujuwa nani atatoka nani atabaki, baada ya comments nyingi za Majaji na hawa ndiyo waliongia kwenye Kumi na Nne Bora ya BSS Second Chance 2011.
1. Beatrice William
2. Bella Kombo
3. Chiby Dayo
4. Hajji Ramadhan
5. Imani Lisu
6. Mary Banyukwa
7. Mary Lucas
8. Mwapwani
9. Rogers Lucas
10. Sarafina Mshindo
11. Shaffi Mohamed
12. Waziri Salum
13. Lulu Abdul
14. Juma Hussein



Comment on this Highlight