Highlight » Ni TOP 5 BSS Second Chance

Ni TOP 5 BSS Second Chance

Tuesday September 20, 2011 1:09 AM BT

image

Ni TOP 5 BSS Second Chance
Hatimaye shindano la BSS Second Chance wiki hii limeingia kwenye TOP 5 ambapo washiriki watano ndiyo wamefanikiwa kufikia nafasi hizo.

Washiriki waliongia TOP 5 ni Bella Kombo (Mwanamke pekee aliyebaki), Chibby Dayo, Hajji Ramadhani, Waziri Salum na Lucas Rogers.

Wakiongea kwa nyakati tofauti wakali hao watano kila mmoja aliwashukuru Watanzania waliofanikisha mafanikio yao.

“Napenda kuwashukuru Wapenzi na washabiki wangu wooote kwa kunifanya kufika 5 Bora, sina cha kuwalipa ila zaidi kuwafanyia mambo mazuri wanayopenda” alisema Bella Kombo.

Waziri Salum nae aliwashukuru Watanzania wote kwa mchango wao kwa hali moja ama nyingine kumfikisha alipo.

Rogers Lucas naye alisema hana la zaidi bali hatawaangusha wote waliomfikisha hapo

Shindano la BSS Second Chance 2011 limeingia kwenye hatua ya fainali mara baada ya mmoja wa washiriki Beatrice George kuyaaga mashindano usiku wa Juzi.



Comment on this Highlight