Highlight » Sarafina na Mary Lucos waaga Mashindano

Sarafina na Mary Lucos waaga Mashindano

Tuesday September 13, 2011 6:24 PM BT


Sarafina na Mary Lucos waaga Mashindano.

Washiriki wawili wote wakiuwakilisha Mkoa wa Dar Es Salaam, Sarafina Mshindo na Mary Lucos usiku wa Jana waliyaaga mashindano ya BSS Second Chance mara baada ya kutolewa kwenye mchujo.

Ilikuwa ni usiku wa huzuni kwa washiriki wote kuagana na wenzao ambapo kila mmoja alitoa machozi, lakini kwenye mashindano kuna kushinda na kushindwa.

Lilianza jina la Sarafina Mshindo kutajwa kama mmoja wanaotoka usiku huo, lakini bila kutegemea Jaji Master Jay naye pia alitaja jina la Mary Lucos ambapo kwa masikitiko makubwa ya kuagana na wenzie walitoa machozi.

Kila mmoja kwa wakati wake akiongea na Bongostars.com alisema ya kuwa kwenye mashindano yoyote kuna kushinda na kushindwa hivyo basi wanachukulia kutolewa kwao kama sehemu ya mashindano.

“Kwa Moyo mmoja kabisa nakubaliana na matoke ya leo, nawashukuru wapenzi na washabiki wangu kwa kunipigia kura mpaka kufikia hapa nawaomba wasubirie ujio wangu, pia nitakuwa mchoyo wa fadhila iwapo sitawashukuru Benchmark na uongozi wote chini ya Madame Rita kusema kweli nashukuru sana kwa kunianzishia njia” alisema Mary

Naye Sarafina ambaye alikuwa ni mmoja wa wanamuziki waliowahi kuimba na Akon katika kutunga wimbo wa Afrika kwenye Fainali za Kombe la Dunia mwaka jana alisema anashukuru washabiki na wapenzi wake kwa kumfikisha hapa alipo.

“Sina cha kuwapa zaidi ya Asante na pia kuwaahidi sitawaangusha” alisema Sarafina

Washiriki wote waliagwa kama ilivyo ada kwenye usiku wa Eviction Party pale Mbalamwezi.



Comment on this Highlight