Highlight » Washiriki Kutumbuiza Mzalendo Wikiendi Hii

Washiriki Kutumbuiza Mzalendo Wikiendi Hii

Thursday August 25, 2011 7:44 AM BT


Washiriki wa BSS Second Chance walioingia Kumi Bora wataufanikisha usiku wa Flava Night Jumamosi hii kwa kutumbuiza ndani ya ukumbi wa Mzalendo Pub.

DJ maarufu Boniventure Kilosa (DJ Venture) alisema wameamua kufanya hivyo baada ya maombi ya wapenzi wengi kuomba irudiwe.

‘Unajuwa hawa washiriki walikuwa hapa wiki mbili zilizopita, lakini kutokana na wapenzi wetu kufurahishwa na performance yao basi maombi yaliongezeka kutaka warudie tena, hivyo basi usiku wa tarehe 27 Jumamosi tutakuwa nao tena, naomba wapenzi wengi wajitokeze” alisema Venture

Pia endelea kutega sikio usikie ni sehemu zipi wapenzi hao wataendelea kutumbuiza katika sehemu mbali mbali za Tanzania.



Comment on this Highlight