Highlight » Waziri apewa Uongozi Kama Onyo

Waziri apewa Uongozi Kama Onyo

Wednesday August 24, 2011 10:22 AM BT
Waziri Salumu mshiriki ambaye wiki iliyopita tuliona kituko chake cha kurushiana maneno na Sarafina Mshindo kikimpelekea kupata karipio kali toka kwa Mwalimu Noah, wiki hii wamemuweka kama kiongozi wa Academy makusudi kwa ajili ya kumfwatilia mwenendo wake mara baada ya tabia aliyoionyesha wiki iliyopita. Waziri ambaye aliomba...

image

Waziri Salumu mshiriki ambaye wiki iliyopita tuliona kituko chake cha kurushiana maneno na Sarafina Mshindo kikimpelekea kupata karipio kali toka kwa Mwalimu Noah, wiki hii wamemuweka kama kiongozi wa Academy makusudi kwa ajili ya kumfwatilia mwenendo wake mara baada ya tabia aliyoionyesha wiki iliyopita.

Waziri ambaye aliomba msahama kwa kosa alilotenda na kusema ni shetani alimpitia na hatarudia tena, pia kumuomba msamaha Sarafina ambaye alikubali msamaha wa Waziri Moja kwa Moja.

‘Kwanza napenda kumuomba msamaha Sarafina kwa kilichotokea, najuwa nimekosea, pili napenda kuwaomba msamaha washiriki na wapenzi wangu wote bila kusahau Mwalimu Noah wa Academy kwani yeye ndiye anatufunza tabia’ alisema Waziri

Sarafina ambaye kwa namna moja ama nyingine alitumia maneno makali kumchokonoa Waziri naye aliomba msamaha kwa kitendo hicho.



Comment on this Highlight